Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
KIPA wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Ivo Philip Mapunda anakaribia kujiunga na timu ya AFC Leopards ya Kenya inayoshiriki Ligi kuu ya nchi hiyo (KPL).
Akizungumzia usajili wake AFC, Mapunda amesema, Ligi ya Kenya imekuwa na neema kwake kwani kujiunga na timu hiyo kubwa nchini humo ni faraja kwake.
Anasema AFC na Gor ni sawa na Simba na Yanga hivyo anajisikia furaha kucheza kwenye vilabu vikubwa katika ukanda huu, Mapunda alitemwa na Simba wakati wa usajili wa dirisha dogo, akajiunga na Azam ambayo nayo imetangaza kumtema