Machapisho

YAMMY AMFUKUZISHA MKE KWA BARNABA

Picha
Baada ya Barnaba kuachia picha za wimbo mpya akiwa na yule bint kitovu nje Yammy tz, huku Yammy akiwa nusu uchi na mchupi kama mcheza X, mke wa Barnaba Raya (Pichani) anayesifika kwa ubabe ameshindwa kuzuia povu lake amekimbia nyumbani na cm hapokei Picha iliyozua gumzo na Sms Raya aliyomtumia Barnaba nmekuekea hapo chini kwenye comments. Hizi couple za wasanii haziish vituko aisee

KOCHA MPYA WA TABORA UNITED KUFUNGASHA VIRAGO

Picha
Kocha mpya wa Klabu ya Tabora United, Denis Laurent Goevec anatarajia kuondoka klabuni hapo baada ya kutoridhishwa na mazingira ya kazi, Denis Laurent Aliamini Mazingira ya Tabora ni Kama ilivyo Dar Es Salaam. Huku CEO wa klabu hiyo Thabithy Kandoro ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake Baada Ya Mambo Ndani ya Timu Kuto Kwenda Katika mpangilio Mzuri wa Kumfanya Afanye Majukumu yake. Pia Baadhi ya wachezaji wamegomea Mazoezi wakishinikiza kulipwa madeni yao Wanayo Yadai kwa Muda Sasa. Muda wowote Masoud Djuma Irambona anaweza akatangazwa kama kocha mkuu wa Tabora United, Masoud Djuma Ambaye Hapo Awali Alienda Tabora United Kama Msaidizi wa Kocha Denis Laurent Ambaye Anaondoka Klabuni Hapo Kutokana na kutoridhishwa na Mazingira ya Kazi.

TAJIRI SIMBA AZUIA KIBU KWENDA YANGA

Picha
Na Shafih Matuwa Habari njema kwa mashabiki wa Simba SC au maarufu kama Wekundu wa Msimbazi kwamba mchezaji wao kipenzi Kibu Denis "Mkandaji" sasa anaweza kubaki kwenye kikosi hicho msimu ujao. Taarifa za ndani zinasema kwamba mmoja kati ya matajiri wa klabu hiyo ameweka mzigo wa fedha mezani na amepanga kumbakisha kikosini kwa kumpa mkataba wa miaka miwili. Na tayari uzushi kwamba anaenda Yanga zimezimwa na presha ya mashabiki wa Simba zinaonekana kuisha, huku mashabiki wa Yanga roho zinawauma waliposikia tajiri huyo amezima jaribio la Kibu kwenda Yanga Kibu Denis anaweza kubaki Simba

GUEDE AENDELEA KUCHEKA NA NYAVU

Picha
Yanga SC imeendelea kuchanja mbuga baada ya jioni ya leo kuilaza Mashujaa FC bao 1-0 katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma mchezo wa Ligi Kuu bara. Kwa ushindi huo Yanga inazidi kuongoza ligi ikiwa na alama 65 ikisaliwa mechi. 4 kukamilisha Ligi hiyo huku Mashujaa ikiwa kwenye hali mbaya. Bao pekee la Yanga limefungwa na Joseph Guede dakika ya 41 huku akiwa na mwendelezo mzuri wa kucheka na nyavu 𝗚𝗨𝗘𝗗𝗘 𝗢𝗡 𝗙𝗜𝗥𝗘 Katika michezo (5) ya mwisho ya Yanga ligi kuu yenye sawa na points (15) ambapo Yanga wamepata points (13), Joseph Guede amechangia points (12)  Na anafunga magoli muhimu tu  Mechi (6) za mwisho alizocheza Guede : ◉  vs  Singida Fountain Gate — ⚽⚽ ◉  vs  Simba Sports Club — ⚽ ◉  vs  JKT - Aligongesha mwamba  ◉  vs  Coastal Union — ⚽ ◉  vs  Tabora United (FA) — ⚽ ◉  vs  Mashujaa FC — ⚽ '

KUELEKEA FAINALI LIGI YA MABINGWA, AHLY YAOMBA UFAFANUZI

Picha
Kuelekea Mchezo wa Fainali ya kwanza CAF Champions league kati ya Esperance na Aly Ahaly Uongozi Wa Aly Ahaly umeomba ufafanuzi CAF juu ya mambo muhimu Kwao kabla ya Mchezo huo. Aly Ahaly wamesema awatoitaji mwamuzi yeyote kutokea kaskazini mwa Africa kusimamaia mchezo huo. Lakini pia wameuliza juu ya utendaji kazi Wa VAR wanataka VAR dabithi. Lakini pia Wameomba kutafutiwa ulinzi imara Kwa ajili ya kulinda Timu Yao, viongozi na mashabiki wao ambao watasafiri Kutoka Misri Mpaka Tunisia. Lakini pia wanataka kujua kuhusu mgawanyo Wa Ticket amabzo zitauzwa ili kupata idadi sawa ya mashabiki. Mchezo utachezwa may 18 /5/2024 Tunisia na Fainali ya pili itachezwa May 25/5/2024 Misri

RULANI MOKWENA AKATAA OFA LUKUKI KUBAKI SUNDOWNS

Picha
Kocha mkuu wa Mamelodi Sundowns Rulani Mokwena anasema alikataa ofa nyingi za kuwania mikoba ya Wabrazil, kufuatia kukatishwa tamaa kwao katika Ligi ya Mabingwa wa CAF. "Nataka kuwa katika klabu hii. Ndio maana nilisaini mawasiliano ya miaka minne. Ingawa nilikuwa na klabu kubwa katika hadhi hiyo zinazotoa ofa na nilichagua kuwa nataka kubaki Sundowns. Sikuchagua hilo kwa sababu nilikuwa nilichagua ile ya kura, (kwa sababu) ya mazungumzo na familia yangu, na klabu, na familia ya Motsepe na pia na wachezaji," Mokwena aliwaambia waandishi wa habari. "Na hivyo nia yangu ni kuwa hapa na kujaribu kufanya niwezavyo kila siku ili kutoa kombe la Ligi ya Mabingwa." "Lakini kiukweli soka ni mchezo wa biashara na unaozingatia matokeo na sifanyi maamuzi hayo kuhusu kocha yupi abaki au aende kocha yupi lakini nikiwa hapa klabu itajua nitatoa. 150% na kama 150% haitoshi, kama leo, nitatoa 200% wakati ujao," Mokwena alisema.

ZUCHU ADAI HARMONIZE AMEBAKIA KUCHAMBANA TU

Picha
Mwimbaji wa Bongofleva, Zuchu amemtolewa uvivu Harmonize na kusema alichobakiza ni vichambo tu!. Kauli ya Zuchu inakuja baada ya Harmonize kuonekana kukejeli malalamiko ya mrembo huyo dhidi ya Diamond Platnumz. "Harmonize huna hit mjini, una kazi ya kuchambana tu...." ameandika Zuchu katika Insta Story na kuongeza. "Baba mzima kazi kudandia visivyokuhusu, mwanamke wako yupo busy kuomba nafasi kwa huyo anayejifanya nusu yako shenzi" - Zuchu.