YANGA WAAHIDI USHINDI KWA MEDEAMA

Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM

YANGA SC imeondoka leo kuelekea Ghana tayari kabisa kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Medeama, hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mabingwa hao wa bara na Ngao ya Hisani, wameondoka na wachezaji wao wote isipokuwa Vicent Bossou na Hassan Kessy, Akizungumza na mtandao huu, kocha wa Yanga Mholanzi Hans Van der Pluijm ameahidi ushindi katika mchezo huo.

Awali Yanga ililazimishwa sare ya kufungana 1-1 katika uwanja wake wa nyumbani wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo itakuwa na kazi ya ziada ili angalau kuchomoza na ushindi ili kufufua matumaini ya kutinga Nusu fainali.

Katika kundi A, Yanga inashika mkia ikiwa na pointi moja wakati TP Mazembe ya DRC inaongoza kwa kukusanya pointi 7, Mo Bejaia wana pointi 5, wakati Medeama wana pointi 2 tu