Na Mwandishj Wetu, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya upendezeshaji na mavazi ya Ndulumo Junior Decorative (NJD) ya jijini Dar es Salaam imemteua Mtendaji mkuu wa Mambo Uwanjani Blogspot Prince Hoza kuwa balozi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akizungumza leo na mtandao huu, Mkurugenzi wa NJD Group Elias Januari amesema kampuni yake imeamua kumteua Hoza kuwa balozi wao kutokana na kuridhishwa na utendaji wake hasa katika mbao za matangazo.
"Hoza atatusaidia katika kuitangaza kampuni yetu kupitia blogu yake, Hoza pia ana kurasa yake katika gazeti la Msimbazi hivyo tumeona bora tufanye naye kazi", alisema Januari.
Kwa sasa NJD wana T: Shirt zao zinazopatikana maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na zikiuzwa kwa bei ya Tsh 15, 000 na 10, 000 zikiwa katika kiwango cha ubora wa juu, Naye Prince Hoza amefurahishwa na uteuzi huo akiamini atafanya kazj na kampuni hiyo, Hoza sasa atakuwa akiinadi kampuni hiyo nchi nzima.
T Shirt zao zenye majina ya Usi4C Nikuamini na Be Distinctive