Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
KLABU bingwa ya soka Afrika mashariki n kati Azam FC imetangaza kuwaacha wachezaji wake sita wakiwemo watatu wa kimataifa kwa madai ya kushuka viwango vyao.
Azam imewaacha makipa Ivo Mapunda na Khalid Mahadhi ambao hawakuwa na nafasi katika kikosi hicho, Mapunda aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Simba, alicheza mechi moja tu.
Wengine walioachwa ni mabeki Racine Diof raia wa Senegar na Said Morad, pia imewaacha washambuliaji wake Didier Kavumbagu raia wa Burundi na Alan Wanga raia wa Kenya.
Kutemwa kwa wachezaji hao kunahirahisishia klabu ya Simba kuwanasa Kavumbagu na Morad ambao ilikuwa ikiwahitaji kwa udi na uvumba, Morad pia anatakiwa na Mbeya City ya jijini Mbeya