CHANONGO ASAINI MIAKA MIWILI MTIBWA SUGAR

Na Ikram Khamees, MOROGORO

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na Stand United, Haroun Chanongo amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro.

Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar Jamal Bayser amesema wameamua kunsaini Chanongo kutokana na umuhimu wake katika kikosi chao, Chanongo amekatisha mkataba wake na Stand kufuatia mgogoro ulioitokea timu hiyo iliyogawanyika makundi mawili.

Awali Chanongo na mwenzake Abuu Ubwa wlaisaini mikataba mipya chini ya uongozi wa Stand Kampuni, lakini baadaye Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF likairudisha timu hiyo chini ya uongozi wa wanachama kitendo kilichopelekea wachezaji hao kutupiwa virago