MEXIME ATIMKIA KAGERA SUGAR

Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM

KLABU ya Kagera Sugar ya Misenyi Bukoba mkoani Kagera imefanikisha kumnyakua kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime na kumtangaza kama kocha wake mkuu.

Taarifa zenye uhakika zilizothibitishwa na mkurugenzi wa Kagera Sugar Mohamed Hussein amesema ni kweli timu yake imemsainisha Mexime na sasa atakuwa kocha mkuu wa Kagera Sugar  hata hivyo Mexime anarithi mikoba ya Adolf Rishard ambaye alikuwa kocha wa timu.

Naye msemaji wa Mtibwa Sugar Tobias Kifaru amekiri kuondoka kwa Mexime lakini amedai yupo jijini Dar es Salaam wakitafuta eneo la kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, Mambo Uwanjani inafahamu kuwa Mtibwa Sugar iko katika mazungumzo ya mwisho na Salum Mayanga ili aje achukue nafasi ya Mexime, Mayanga alikuwa kocha wa Prisons