Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
NAHODHA na mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco "Adebayor" amekataliwa na makocha wapya wa timu kutoka Hispania.
Bocco amekataliwa na makocha hao wakidai hana kiwango cha kuichezea timu hiyo chini yao, wakati Bocco akikataliwa, viongozi wa timu hiyo wanahaha kutaka kumuombea abakishwe lakini wazungu wamemgomea kabisa.
Jonas Garcia raia wa Hispania na mwenzake Zeben Hainendez wamemtosa mshambuliaji huyo aliyewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi kuu bara, Bocco ni mmoja kati ya washambuliaji tegemeo lakini wazungu wanasema hana lolote na hakustahili kucheza Azam na ndio maana timu hiyo haina mafanikio