Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MKUU wa kitengo cha Mawasiliano na Habari wa Simba SC Haji Sunday Manara ameisifu klabu ya Yanga ambao ni mahasimu wao wa jadi.
Akizungumza na mtandao huu kabla ya kukwea pipa kuelekea nchini India kufanyiwa matibabu ya jicho lake la upande wa kushoto ambalo limepoteza uwezo wa kuona, ameishukuru Yanga ambayo imemchangia baadhi ya fedha kwa ajili ya matibabu.
Yanga kupitia kundi lake la mashabiki wamemchangia msemaji huyo wa Simba kiasi kisichopungua milioni 1, msemaji wa Yanga Jerry Muro ndiye aliyejitokeza na kumkabidhi kiasi hicho cha fedha