BATAROKOTA WA KTMA AKAMATWA KWA UTUPAJI TAKA MOROGORO

Na Ikram Khamees, MOROGORO

MSANII wa muziki wa asili ambaye mwaka 2014 aliingia kwenye kinyang' anyiro cha kuwania tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Award (KTMA)  na wimbo wake wa Kwejaga Nyangisha, Batarokota, juzi alikamatwa na mgambo wa manispaa wa mji wa Morogoro kwa kosa la kutupa taka.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo, Batarokota alionekana akitupa chupa ya maji ndipo askari hao wa mgambo waliokuwa wakikatiza mitaani walipomuona na kumtia hatiani.

Hata hivyo msanii huyo alishikiliwa kwa masaa mawili na kuachiwa baada ya kutetewa na mwenyekiti wa mtaa wa Nane Nane Bi Ruth Kipawa kumuombea msamaha na kuachiwa huku akitakiwa kuhamasisha wananchi wasitupe takataka hovyo kwani ni kosa kisheria