Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZAJI wa zamani wa Small Simba ya Zanzibar na AFC ya Arusha Mossi Shaaban amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya Kisukari kwa muda mrefu.
Kiungo wa zamani wa Mlandege na Yanga SC Deogratus Lucas ameitonya Mambo Uwanjani kwamba marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari kwa muda mrefu na kusababisha akatwe mguu wake mmoja.
Lucas amedai Mossi amefariki leo na mipango ya mazishi inapangwa na wanafamilia, mchezaji huyo amewahi kutamba na Small Simba timu ambayo ilikuwa ikitikisa soka la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla