Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM
MEDEAMA ya Ghana jioni ya leo imeilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 Yanga SC ya Tanzania mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema dakika ya kwanza kipindj cha kwanza likifungwa na mshambuliaji wake hatari Mzimbabwe Donald Ngoma, Lakini Medeama walisawazisha katika kipindi hicho cha kwanza na kuwa sare.
Matokeo hayo yalibaki hivyo hadi mwisho wa mchezo licha ya mwamuzi kuongeza dakika tano za nyongeza, Kwa matokeo hayo Yanga sasa imepoteza matumaini ya kusonga mbele kwani ina pointi moja wakati Medeama wana pointi mbili na TP Mazembe wanabaki kileleni na pointi zao sita na Mo Bejaia wana pointi nne, Yanga watarudiana na Medeama Julai 26