KIPUTE YANGA NA AZAM AGOSTI 17

Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM

MTIFUANO wa Ligi kuu bara unatarajia kuanza mwezi ujao, lakini kutakuwa na mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Yanga SC na Azam FC Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mechi hiyo ya Ngao itakuwa ya nne kwa miamba hiyo huku mara zote Yanga ikitoka na ushindi, Ikumbukwe mwaka jana Yanga ilitwaa Ngao kwa kuifunga Azam kwa penalti 8-7 baada ya sare ya 1-1.

Mara ya baada ya mechi hiyo ndipo Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara itakapoanza, Je Yanga itaibuka na ushindi katika mchezo huo? au Azam watalipa kisasi! ngoja tuone