MEDEAMA WAONDOKA NA YONDANI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa timu ya Medeama ya Ghana ambayo iliwakazia Yanga na kuilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, wameondoka na jina la beki wa Yanga Kevin Yondani.

Taarifa zenye uhakika kutoka kwe ye benchi la ufundi la timu hiyo zinasema Kevin Yondani amewavutia mno vigogo wa timu hiyo na wako radhi kuimwagia fedha yoyote watakayoitaka Yanga ili waweze kumnasa.

Yondani alicheza vizuri katika mchezo huo ambao uliiwezesha Yanga kupata moja tangu waanze michuano hiyo, Yanga na Medeama watarudiana Julai 26 mwaka huu huko Ghana, matumaini kwa Yanga kusonga mbele bado yapo kwani inahitaji ushindi katika mchezo huo