SHIZA KICHUYA AANGUKA SIMBA MIAKA MIWILI

Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM

LICHA kwamba viongozi wa Simba wanafanya siri, Lakini taarifa zinavuja kwamba winga wa Mtibwa Sugar ya Morogoro Shiza Ramadhan Kichuya amesaini miaka miwili tayari kabisa kukipiga na Wanamsimbazi.

Mtibwa Sugar jana ilifikia makubaliano na Simba na kumruhusu winga huyo teleza ambaye leo ametangazwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa Tanzania.

Kusajiliwa kwa Kichuya na klabu ya Simba kunaifanya Mtibwa Sugar iondokewe na wachezaji wake watatu ambao wote wanajiunga na Simba, wachezaji wengine waliohamia Simba ni Muzamil Yassin, Mohamed Ibrahim na Kichuya