Na Mwandishi Wetu, DODOMA
MSANII maarufu wa filamu hapa nchini Jacquliene Wolper anayeunda kundi la Bongomovie hatimaye amerejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuachana na swahiba wake Waziri mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa aliyejiunga na Chadema.
Awali Wolper alijiunga Chadema na katika kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana alikuwa mpiga debe namba moja wa Lowassa aliywgombea urais kupitia Chadema.
Akiwa mjini Dodoma ulikofanyika mkutano mkuu wa CCM ambao ulihitimisha uenyekiti wa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete, Wolper na wengine walitangaza kurejea CCM na kudai upinzani ni sawa na kibudu.
Pichani chini Wolper akionekana kufurahia kurejea CCM