NDANDA YAZIDI KUJIIMARISHA, YAMNASA TELELA

Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM

TIMU Ndanda ya Mtwara inayoshiriki Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, inazidi kujiimarisha katika usajili baada ya kufanikiwa kumnasa kiungo wa zamani wa Yanga, Salum Telela.

Telela ambaye mkataba wake na Yanga uljmalizika, Na kocha wa Yanga Mdachi Hans Van der Pluijm alikataa kumuongezea mwingine, amejiunga na Ndanda kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Tayari Ndanda ilishafanikiwa kumnasa beki wa Simba Hassan Isihaka, kwa maana hiyo kikosi hicho cha Ndanda msimu ujao kitakuwa tishio, isitoshe Ndanda itafungua dimba kwa kucheza na Simba SC mchezo wa Ligi kuu bara