Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
YANGA SC iliwahi kutamba katika michuano ya kombe la Kagame iliyofanyika nchini Uganda mwaka 1996 na Yanga wakawa mabingwa baada ya kuwachapa SC Villa mabao 3-1.
Katika kikosi cha Yanga wakati huo walikuwa na winga wao machachari ambaye aliacha simulizi Uganda nzima, Edibily Lunyamila alitamba vilivyo kiasi kwamba wafanyabiashara nchini Uganda wakaanza kuandika mabango kwenye biashara zao yenye jina la winga huyo.
Kwakweli alifunika vilivyo kwenye michuano hiyo, Lunyamila alitamba pia kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, Lunyamila alijiunga na Yanga SC akitokea Biashara Shinyanga timu iliyoibukia kwenye ligi kuu ya Tanzania na ikapotea ghafla ikiacha simulizi.
Lunyamila alitamba Yanga lakini baadaye ajaondoka baada ya kukorofishana na viongozi wa Yanga na akajiunga na Malindi ya Zanzibar kisha akasajiliwa na Simba SC ambapo alitamba nayo kabla hajaacha soka.
Lakini kiungo huyo wa pembeni aliwahi kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Ujerumani kwenye timu ya Daraja la nne, hata hivyo Lunyamila alishindwa kuendelea na majaribio baada ya kuambiwa umbo lake ni dogo na alihitaji kuongeza msosi ili awe na nguvu zaidi kwani ligi ya Ujerumani ni ya kutumia nguvu