NGASSA AANZA MAISHA MAPYA MOROKA SWALLORS

Na Mwandishi Wetu, Afrika Kusini

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa hatimaye ameanza maisha mapya katika klabu yake mpya ya Moroka Swallors hasa baada ya klabu yake ya hapo mwanzo ya Free State Stars kupigwa bei.

Ngassa aliyekuwa akiichezea Free State iliyomnunua kwa mkataba wa miaka mitano akitokea Yanga SC ya Tanzania amejikuta akiachana na timu hiyo baada ya kununuliwa na Moroka Swallors timu iliyoshiriki Ligi daraja la pili.

Hata hivyo sasa Moroka itashiriki Ligi kuu ya ABSA ikichukua nafasi ya Free State, Ngassa na wenzake wamejumuhishwa kwenye kikosi hicho ina maana anakuwa mchezaji mpya wa Moroka Swallors ambayo iliwahi kutikisa katika miaka ya 90

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI