Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika, Yanga SC usiku huu wamekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao AS FAR Rabat uwanja wa Stade Olympique mjini Rabat.
Yanga ikicheza vizuri ikitaka kuzuia muda wote Ili wasifungwe, lakini ikakubali kuruhusu goli dakika ya 85 na kufanya mchezo wake wa mwisho dhidi ya JS Kabylie lazima ishinde zaidi ya goli moja huku FAR Rabat ipoteze dhidi ya Al Ahly.
Bao la ushindi la FAR Rabat limefungwa na Anas Bach dakika ya 85, wakati huo JS Kabylie ya Algeria imeshindwa kupata ushindi mbele ya Al Ahly ya Misri kwa kutoka sare ya 0-0.
.
