Timu ya Yanga SC usiku huu imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania bara, Cosmopolitan zote za Dar es Salaam katika uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam mchezo wa kombe la CRDB Cup.
Mchezo ulikuwa wa kuvutia kwani Cosmopolitan ilicheza vizuri na kujaribu kulifikia lango la Yanga mara kadhaa na kuna nyakati kidogo ilikuwa wafunge bao lakini mpira ulienda kugonga mwamba.
Mabao yote ya Yanga walifungwa na winga wao mpya Bubah Jameh dakika ya 13 na 23, kwa ushindi huo Yanga imetinga raundi ya tatu ya michuano hiyo ikiwa ni bingwa mtetezi.

