Yanga wamewasilisha barua kwa Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF kuomba kubadilishiwa mwamuzi atakaechezesha mchezo wa Ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie katika uwanja wa New Aman Complex Zanzibar..
Mwamuzi Jaque Ndala( 34) kutoka DR Congo ndiyo mwamuzi aliyeteuliwa na CAF kusimamia mchezo huo.
Ikumbukwe tu huyu ndiyo mwamuzi aliyewachinja Tanzania dhidi Morocco katika michuano ya AFCON yaliyofanyika nchini Morocco msimu huu .!
Mchezo wa Yanga na JS Kabylie utatoa taarifa kwa umma kuwa Yanga amesonga robo fainali au amesalia Ligi Kuu NBC..
Kama ombi lao litajibiwa basi furaha ya wananchi itarejea kutokana na Jaque Ndala kutokuwa na Imani naye.
