Aliyekuwa Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC, Haji Manara "Computer" amesema bila kuogopa kwamba klabu yake ya Yanga imefeli.
"Yanga msimu huu tumefeli haiwezekani misimu minne robo fainali moja tu, halafu kila msimu kila dirisha tunasajili wachezaji wapya sita saba kila dirisha na kila msimu kocha mpya, hesabu makocha wangapi wamepita baada ya Nabi isitoshe na nimewaambia ukweli hadi Rais unaenda kusajili Mchezaji wa Kimataifa anakaa benchi na wakati mwingine hapenyi hata kwenye Wachezaji 18 wa mechi yaani tunakaa nae Jukwaani sasa kusajili Mchezaji Kimataifa hana uwezo si ni UCHALE huu?”
- Haji Manara, Diwani wa Kata ya Kariakoo na aliyekuwa Msemaji wa Yanga.
