Mechi ijayo ni fainali kwa Yanga, kwanza wanahitaji ushindi ili wafuzu moja kwa moja bila kusubiri matokeo ya mechi ya mwisho, (endapo JS Kabylie atashindwa kumfunga Al Ahly) ,pili Yanga,wakishindwa kumfunga FAR Rabat .
Basi Yanga wapambanie sare kisha wasubiri kushinda mechi yao mwisho ili wafuzu ,au wamuombee mabaya FAR Rabat kwenye mechi yake ya mwisho dhidi ya Ahly, na tatu Yanga wakifungwa basi wasifungwe kwa tofauti ya goli moja maana wakifungwa 2-0, 3-1 na kuendelea mchezo utakuwa umeisha na FAR Rabat watasonga mbele kwa H2H bila hata kusubiri matokeo ya mwisho.
Mechi ijayo ni fainali kwa Yanga,faida kwao ni kwamba FAR Rabat hawatokuwa na mashabiki…..hivyo Yanga wakaze.
