Mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania, Gabriel Geay, amepongezwa kwa kuibuka mshindi na kutwaa medali ya dhahabu katika Mbio za Daegu zilizofanyika Korea Kusini.
Geay alimaliza mbio hizo kwa muda wa saa 2:08:04, akiandika ushindi wake wa pili mfululizo katika mashindano hayo, baada ya mwaka 2025 pia kutwaa taji hilo kwa muda wa 2:05:22.
Miongoni mwa waliompongeza ni Jasmin Kikwete, Balozi wa Utalii na Uwekezaji wa Jumuiya ya Madola na Mkurugenzi wa Blue Visit Tanzania & Zanzibar, ambaye kwa kushirikiana na wadau wengine amekuwa akiunga mkono riadha kupitia dhana ya utalii wa michezo. Ushindi huo unaendelea kuiweka Tanzania kwenye ramani ya riadha kimataifa.
