Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tresor Mputu; Mchezaji bora wa muda wote TP Mazembe

Mwamba huyu hapa Tresor Mputu mabi anatajwa kuwa ndiye mchezaji bora wa muda wote wa TP Mazembe yaani sio Rainford Kalaba au Mbwana Samatta anayeheshimiwa zaidi pale Mazembe. 

Imagine kuna kipindi mzee arsène wenger aliwahi kumuhita kucheza arsenal lakini mwamba alikataa akisema hali ya hewa ya England ni changamoto kwake.

Mputu alijiunga na TP Mazembe mwaka 2002 ambapo alicheza mechi 292 na kufunga magoli 144.

Ameshinda mataji yafuatayo akiwa na TP Mazembe;
1:Caf Champions mara 1 mwaka 2009
2:Caf Super Cup mara 1 mwaka 2010
3:Ligi Kuu ya Congo DRC mara 5
2006,2007,2009,2011 na 2012.

Tuzo binafsi alizoshinda Mputu ni
1:Mchezaji Bora kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika mwaka 2009.

Mchezaji Bora Ligi Kuu ya DR  Congo mara 3; 2007,2009 na 2011.
Tuzo ya mfungaji Bora IFFHS 2007.

Mputu amecheza vilabu viwili tu kwenye career yake ya mpira mwaka 2014 alijiunga na Kabuscorp ya Angola ambapo alicheza mechi 49 na kufunga goli 18 mwaka 2016 akarejea tena TP Mazembe.

Akiwa na jezi ya timu ya taifa ya Leopards, Mputu alicheza mechi 47 na kufunga goli 14.

Maisha yake nje ya uwanja yalikuwa ni ya majivuno sana mfano mashabiki zake walipotaka kumuona Mputu alikuwa hashushi kabisa vioo vya gari yake na hata kumngusa tu ni kosa kubwa.

Rais wa TP Mazembe alimjengea kiwanja chake binafsi cha mazoezi. Kwa ufupi Mputu alifaidi sana pesa za Moise Katumbi haswa.

Kwa ufupi yapo mengi yanayomuhusu Mputu. Next time nitakuletea story yakushindania ufalme kati ya Mputu na Mbwana Samatta ndani ya TP Mazembe.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa