Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imevifungulia viwanja vya Sokoine Mbeya pamoja na Ali Hassan Mwinyi, Tabora kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanya marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Viwanja vyote vipo tayari kutumika kwenye mechi zijazo za Ligi Kuu ya NBC.
Aidha, TFF inaendelea kuzikumbusha klabu kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao vya nyumbani ili michezo ya Ligi ichezwe kwenye viwanja bora vinavyosaidia kuongeza ushindani na thamani ya Ligi.
