Tanzania Prisons yapindua meza kibabe, yaishona Namungo 3-2
Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Namungo FC umetamatika ambao umekuwa wakusisimua baada ya Tanzania Prisons, kufanya comeback ya kishujaa kipindi cha pili na kuibuka na ushindi wa magoli 3-2.
Namungo FC walionekana kuumiliki mchezo mapema baada ya kupata mabao mawili ya haraka kipindi cha kwanza kupitia kwa Cyprian Kipenye aliyefunga dakika ya 36 kwa mkwaju wa penalti huku chuma cha pili kikiwekwa kambani na Fabrice Ngoy dakika ya 43.
Hata hivyo, Tanzania Prisons walirejea kwa nguvu kipindi cha pili na kubadili kabisa mwelekeo wa mchezo baada ya Lambert Sabiyanka alipoanza kupunguza mlima wa magoli dakika ya 49 huku George Mpole akasawazisha dakika ya 71 kwa mkwaju wa penalti na Oscar Mwajanga akafunga bao la tatu la ushindi.
Ushindi huu unaipa Tanzania Prisons alama tatu muhimu katika msimamo wa Ligi hiyo.
