Kiungo mshambuliaji raia wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki, huenda akarejea tena katika klabu yake ya zamani ya Yanga SC kufuatia taarifa zinazozagaa kwamba Yanga wanamrudisha.
Habari za uhakika kabisa kutoka viunga vya Jangwani, Aziz Ki aliyeuzwa kwa klabu ya Wydad Athletic ya Morocco kisha na wao kumuuza Al Ittihad ya Libya, uongozi wa Yanga umeona biashara ya mchezaji huyo haikuwapa amani kwani pengo lake linaonekana dhahiri.
Hivyo kwenye usajili wa dirisha kubwa la Agosti mwaka huu, jina la Aziz Ki litakuwa miongoni mwa wachezaji wapya wa mabingwa hao wa Tanzania bara.
