TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na winga Mrundi, Ndumumwe Mossi dakika ya sita, mshambuliaji Mkongo, Malanga Horso Mwaku dakika ya 17 na beki Kennedy Wilson Juma dakika ya 59, wakati bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na kiungo Raizin Hafidh dakika ya 88.
Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 15 katika mchezo wa tisa na kusogea nafasi ya 10 kutoka ya 13, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 21 za mechi 15 sasa nafasi ya nne.
