Timu ya Singida Black Stars ya Tanzania imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika uwanja wa New Amaan Stadium, Zanzibar usiku huu.
Goli ambalo limewalaza Singida Black Stars limefungwa na Abdenoour Belhocin, nafasi ya Singida Black Stars kusonga mbele ni ndogo sana hivyo kimahesabu imetolewa kama ilivyo Simba SC pia ya Tanzania.
