Timu ya Simba SC usiku huu imeichapa bila huruma timu ya Greenland mabao 3-0 mchezo wa kombe la CRDB katika uwanja wa Meja Isamuyo Mbweni jijini Dar es Salaam.
Greenland inayotoka mkoani Kagera, imecheza vizuri kwani ingeweza kuchakazwa mabao mengi zaidi, lakini iliwachukua Simba kupata bao la kuongoza dakika ya 13 na mshambuliaji Baraka Mwangosi kabla ya beki wa kushoto Anthony Mligo dakika ya 45 kufunga la pili.
Hadi mapumziko Simba walikuwa kileleni kwa mabao hayo mawili, kipindi cha pili Simba walipata bao la tatu kupitia kwa Neo Maema dakika ya 90, kesho watani zao Yanga wataumana na mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu bara wakati huo Ligi daraja la kwanza Tanzania bara, Cosmopolitan uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam
