Wekundu wa Msimbazi, Simba SC usiku huu wamelazimishwa sare tasa 0-0 na Dodoma Jiji FC uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mchezo wa Ligi Kuu bara inayodhaminiwa na benki ya NBC.
Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 23 na michezo 10 ikipanda nafasi moja kutoka ya nne mpaka ya tatu wakati Dodoma Jiji amefikisha pointi 21 ikiendelea kushikilia nafasi ya sita.
Mechi itakayofuata ni watani wa jadi Yanga na Simba itakayopigwa uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar.

