Uongozi wa klabu ya Simba SC umejidhatiti kwamba msimu ujao lazima kikosi chao kirejee kimataifa na kitafika hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika na ikiwezekana kitafika nusu fainali au fainali yenyewe.
Hayo yote yametokana na mabadiliko waliyoyafanya msimu huu hasa katika dirisha dogo baada ya kufanya sajili nzuri, uongozi huo kwa nyakati tofauti wameridhishwa na kikosi chao kilichocheza mechi zote za mzunguko wa pili wa hatua ya makundi Ligi ya mabingwa Afrika.
Kuanzia mchezo marudiano dhidi ya Esperance uliomalizika kwa sare ya 2-2 uwanja wa Mkapa na ule dhidi ya Petro Luanda ulioisha kwa sare ya 1-1 mjini Luanda na huu wa Jumamosi iliyopita Simba ikishinda 1-0 uwanja wa Mkapa.
Simba imeambulia pointi 5 hivyo ni hatua nzuri kwao tofauti na walivyoanza ambapo walipoteza mechi 3 mfululizo, pia uongozi huo wa Simba umeridhishwa na benchi lao la ufundi linaloongozwa na Steve Barker na pia wachezaji wao wapya waliowasajili kwenye dirisha dogo





