Na Prince Hoza Matua
KWENYE hali ya kushangaza, Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji kupitia ukurasa wake wa Instagram amehoji kwenye ukurasa wa Klabu ya Simba kuwa suala la Mabadiliko ndani ya Simba limefikia wapi?
.
Jambo ambalo limewashangaza wengi ni namna ambavyo Mwekezaji huyo amekuja kuuhoji uongozi wa Simba kuhusu suala la Mabadiliko ikiwa naye ni sehemu ya watu wanaohusika na kufanya Mabadiliko ndani ya Simba na huku ikiwa ni siku chache tangu zitoke tetesi za kwamba Bilionea huyo amejiondoa ndani ya Simba.
.
Mo Dewji anaahidi kuwaacha njiapanda mashabiki wa Klabu hiyo juu ya yeye kuwepo Simba na mbaya zaidi anahoji mitandaoni badala ya kuwafuata viongozi wenzake kwenye ofisi zao.
Kwa vyovyote mchakato wa mabadiliko ya klabu ya Simba SC inaonekana kama ya kiini macho na badala yake klabu ya Simba wanatakiwa kuanza upya mchakato, Wekundu hao wa Msimbazi, wameshindwa kukamilisha mchakato wa uwekezaji na kilichobaki ni sinema tu.
Kitendo cha MO Dewji kuhoji mchakato wa mabadiliko unakwendaje wakati na yeye ni sehemu ya viongozi, mchakato wa Simba unaonrkana kufeli kwani unapingana na matakwa ya serikali ambapo
Serikali inavitaka vilabu vya soka nchini vimavyotaka kuingia kwenye mabadiliko waakikishe wawekezaji wawe watatu na kuendelea na si mmoja kama ambavyo wanavyafanya Simba SC.
Mchakato wa mabadiliko wa klabu ya Simba unaendeshwa na mtu mmoja ambaye ni Mohamed Dewji "MO Dewji", Simba walitembea na mwekezaji mmoja aliyebahatika kubadili katiba ambayo inamfanya kuwa mmiliki na pia kuunda Bodi ya Wakurugenzi.
Pia mwekezaji MO Dewji, ameajiri CEO wa klabu halafu baadaye tunamsikia mwekezaji anaulizia mchakato wa mabadiliko kwa viongozi wa klahu, siyo siri mchakato wa mabadiliko wa Simba awamu ya kwanza imefeli na kinachopaswa kwa klabu hiyo ni kuanza mchakato upya.
Itakuwa vizuri sana endapo uongozi wa Simba wataanza upya mchakato huo wa mabadiliko na pia kubadili katiba ya klabu ambayo itampa nguvu mwenyekiti wa klabu hiyo Ili awe pia mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.
Klabu inatakiwa kubaki na Hisa, asilimia 51 na zilizobaki asilimia 49 wapewe wawekezaji, MO Dewji anajua fika mchakato wa mabadiliko wa Simba unatakiwa kuanza upya na ndio maana amehoji.
Ule mchakato walioufanya hapo awali umegoma na serikali imeukataa ni bora waanze upya, nahisi viongozi wa Simba chini ya Murtaza Mangungu unafungua milango ya kuanza upya na ndio maana wameanza na suala la kuingiza wanachama wapya.
Uongozi wa Simba unapaswa kuwaiga Yanga katika suala la transformation, kwani Yanga walifanya mchakato wao bila kushawishiwa na GSM ambaye ndiye mfadhili kama ilivyo kwa MO Dewji.
Yanga waliamua kwenda Hispania kujifunza uwekezaji na wakaanza mchakato wao vizuri pasipo kulumbana, wanachama wa Yanga SC walifurahishwa na asilimia 51 ambazo wamepewa wanachama na pia kufurahishwa wawekezaji kupewa 49.
Bodi ya Wakurugenzi ya Yanga itaongozwa na Rais wa klabu, tofauti na ilivyo kwa Simba ambapo mwenyekiti wa klabu anageuka kama mwanachama wa kawaida ambaye hajui chochote kuhusu maendeleo ya klabu yake.
Simba inatia huruma pale mwenyekiti wa klabu yake anaposhambuliwa na mashabiki wakishinikiza ajiuzuru, mashabiki hao waliomshambulia mwenyekiti wa Simba wanadai ni yeye ni tatizo kwa Simba kutofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.
Lakini kama wangeujua ukweli wasingejaribu hata kidogo kumshambulia kwa sababu mwenyekiti wa Simba ni kama wao tu hajui chochote, viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi inayoongozwa na MO Dewji ndio inayotekeleza yote ya Simba katika suala la kufanya usajili na maandalizi ya timu na siyo mwenyekiti wa klabu.
ALAMSIKI
