Wekundu wa Msimbazi, Simba SC usiku huu wameongeza alama tatu muhimu baada ya kuilaza KMC FC mabao 2-0 uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu bara.
Kwa matokeo hayo sasa Simba inapanda hadi nafasi ya sita ikiishusha Dodoma Jiji yenye pointi 17 wakati Simba inafikisha pointi 19 ikicheza mechi 8.
Mabao ya Simba yamefungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 37 na Libasse Gueye dakika ya 46, Simba sasa wanaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika Jumanosi dhidi ya Stade Malien ya Mali uwanja wa Mkapa.
Wakati huo huo Singida Black Stars imeifunga Fountain Gate bao 1-0 na kufanikiwa kufikisha alama 12 ikikaa nafasi ya 13 toka mkoani ikiwa imecheza mechi 8.
