Uongozi wa Simba SC umeiandikia barua Bodi ya Ligi (TPLB) kutaka kujua kwanini taarifa ya kuhamisha uwanja kutoka Benjamin Mkapa kwenda Amaan Complex ilitolewa kwanza na Afisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe badala ya Bodi ya Ligi TPLB na Bodi ikaja kutangaza siku yake ya pili ya Februari 16, 2026 baada ya Ali Kamwe kutangazwa jana yake Februari 15, 2026.
Katika barua hiyo pia Simba Sports Club imehoji kanuni ipi imetumika kuhamisha uwanja maana ilitakiwa taarifa ya kuhamishwa kwa uwanja itoke kabla ya siku 21 kama kanuni inavyosema, taarifa ya kuhamishwa uwanja ilipaswa kutoka siku 21 kabla ya siku ya mechi husika.
