Mchambuzi wa soka nchini Shafih Dauda amewaambia mashabiki wa Simba waliomzonga na kumshambulia mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu jioni ya leo uwanja wa Mkapa wakati Simba inacheza na Esperance, watamuomba radhi kwani Mangungu ahusiki la lolote kuhusu Simba isipokuwa wakiwajua wahusika watagundua kwamba Mangungu hana kosa lolote.
Dauda ameyasema hayo akizungumza na Sports Extra ya Clouds FM ambapo amedai kwamba mashabiki hao wa Simba hawajatumia hekima na pia dharau kwa timu ya Esperance.
"Mashabiki wa Simba hawajaiheshimu Esperance kwani ni miongoni mwa timu kubwa na bora barani Afrika, wenzao Yanga jana wameiheshimu Al Ahly na ndio maana sijaona mashabiki wa Yanga wakiijia juu timu yao kwa sare ya 1-1 wakiiua fika Ahly ni timu kubwa, lakini Simba leo heshima haijawekwa kwa Esperance, sare ya 2-2 licha ya kuongoza 2-0 kipindi cha kwanza, mashabiki wametaka kumpiga mwenyekiti wa klabu", alisema Dauda.
