MENEJA Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, ameshangazwa na kauli ya mchambuzi Hans Raphael aliyedai kuwa Elie Mpanzu ana mapenzi na Yanga SC licha ya kucheza Simba.
“Nilimsikia mchambuzi wenu akisema mchezaji wetu anacheza tu Simba, lakini ana mapenzi na Yanga. Unawezaje kuthibitisha hilo?”
Ahmed amesema kauli hiyo si sahihi na imemkosea mchezaji, hasa kwa kipindi anachopitia.
“Amemkosea sana mchezaji, ile sio sentensi ya kuzungumza hadharani. Mpanzu ametoka kufiwa na mtoto wake hivi karibuni, sio rahisi kwake. Anapitia nyakati ngumu.”
