Rais wa Shirikisho la Soka nchini Cameroon, Samuel Eto’o, amewasili Dar es Salaam leo, tayari kwa mkutano wa kamati ya utendaji ya CAF, utakaofanyika kesho, Februari 13, 2026.
Eto’o ni miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo ambao tayari wamekwishashawasili nchini kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika, kwa ajili ya mkutano huo unaolenga kujadili na kuimarisha maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika.


