Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Le Havre, Mbwana Samatta ameendelea kuandamwa na ukame wa mabao akiwa na siku 343 bila kuzifumania nyavu tangu alipofunga kwa mara ya mwisho mnamo March 2 mwaka jana kwenye mchezo wa Greek Super League wakati akiitumikia PAOK .
Takwimu zake za klabu na timu ya taifa tangu alipofunga kwa mara ya mwisho mnamo March 2, 2025.
1303 - Minutes
23 - Games played
00 - Goals
01 - Assists
Kati ya washambuliaji wa kati waliopiga mashuti 20+ yanayojumuisha yaliyolenga goli na yasiyo lenga goli katika ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1) msimu huu, ni Samatta pekee ambaye bado hajafunga bao mpaka sasa .
Samatta akiwa na Le Havre katika Ligue 1 msimu huu hadi sasa .
◉ 14 - Games
◉ 43 - Touches in opp. box
◉ 21 - Shots
◉ 07 - Shots on target
◉ 00 - Goals
◉ 00 - Assists
