Kwa hali jinsk ilivyo inaonekana wazi kocha mkuu wa Yanga SC Pedro Goncalves raia wa Ureno ameonyesha wazi wazi kuridhishwa na uchezaji wa beki wa kushoto wa klabu hiyo Chadrack Boka na amekuwa akimpanga kwenye baadhi ya mechi za timu hiyo.
Ingawa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo wanampenda sana beki wao mwingine Mohamed Hussein "Tshabalala" na wamekuwa akishinikiza aanzishwe kwenye kikosi chao, lakini Pedro amekuwa akimpanga Boka kwakuwa mapenzi yake yapo kwa beki huyo raia wa DR Congo.
Yanga ilikuwa na kocha mkuu aitwaye Roman Folz ambaye alipoanza kuinoa Yanga alikuta timu ina kikosi kilichoenea viungo mahiri akiwemo Duke Abuye ambaye alikuwa panga pangua, lakini kocha huyo alianza kumuamini Aziz Andabwile na akawa kwenye kikosi cha kwanza.
Mashabiki wa Yanga walianza kulalama wakitaka Andabwile akae benchi huku Duke Abuye pamoja na kiungo mpya Mousa Balla Conte waanze, lakini Folz humwambii kitu kwa Andabwile hivyo ndivyo kwa Pedro kumwamini Boka.
