Anaandika Mdau
Dhahiri fujo alizofanyiwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu ni mpango uliofeli ambao umeratibiwa kishamba, swali ni nani aliyepo nyuma ya huu USHAMBA?
Dhahiri kuna mashabiki wameandaliwa kumfanyia fujo Mwenyekiti wa klabu bila sababu ya msingi. Manake kama wangekuwa na hasira na viongozi kwanini Cresentius Magori Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu hakufanyiwa fujo ilihali nayeye alikuwepo Taifa na akatoka kama mfalme?
Bodi ya Wakurugenzi ya Simba ndiyo KILA KITU katika kuiongoza klabu kwa sasa kwa mujibu wa makubaliano ya upande wa wanachama na upande wa MO na Mwenyekiti wake ameteuliwa na MO.
Mwenyekiti wa Klabu ambaye anatokana na wanachama HANA LOLOTE mbele ya Mwenyekiti wa Bodi, kama kweli mashabiki wana hasira na viongozi kwanini wambague Mwenyekiti wa Bodi na yule wa Wanachama? Wangeshambuliwa wote kuonyesha hasira zao kwa uongozi, lakini hili lilifanyika ni Ushamba ulioratibiwa Kishamba na wajinga ambao hawana wanalojua, waliotekeleza ni wapuuzi ambao wametumika kama TOILET PAPER tu.
Kuna watu wanajidanganya kwamba Mangungu atatolewa kwa vurugu ili wafanya wanachotaka, wasahau kwakuwa ishu sio Mangungu, Serikali ndiyo iliyotoa maagizo ya marekebisho ya Katiba ili klabu ijiendeshe, najua hapa ndipo kuna MZIZI WA TATIZO hawa vijana wanatumika tu.
Sasa upande wa Mangungu ukipanga vijana kushambulia Mwenyekiti wa Bodi itakuaje? Punguzeni ushamba hizi mambo za kizamani sana na nyakati hizi haziwezi kufanya kazi.
Timu lenu lina alama 1 na haliwezi kwenda popote, NBC PL ina “wenyewe” tayari na washakaa pahala pao, nyinyi mnatengenezeana watu wa kufanya vurugu, ujinga kiasi gani. Mnadhani eti Mangungu ndo ataonekana tatizo ili mtu au watu fulani waonekane wazuri, upuuzi.
Subirini mkutane nao GONGOWAZI wakuchapeni tena halafu ubingwa mkose, muone kama hawa mnaowatuma hawajawageuka.
