Mwanariadha wa Tanzania, Gabriel Geay, ameibuka mshindi katika mbio za Daegu Marathon zilizofanyika Korea Kusini, na kutwaa medali ya dhahabu.
Geay alimaliza mbio hizo kwa muda wa saa 2:08:09, akimshinda mpinzani wake wa karibu kutoka Ethiopia, Chimdesa Gudeta.
Geay amefanikiwa kutetea ubingwa wake, kwani mwaka 2025 alishinda mbio hizo zilizofanyika huko huko Korea Kusini.
Mwanariadha mwingine wa Tanzania, Josephat Gisemo, alimaliza nafasi ya tatu na kutwaa medali ya fedha baada ya kutumia muda wa saa 2:08:17.
Ushindi wa wanariadha hao unaendelea kuthibitisha nafasi ya Tanzania katika mbio za kimataifa na nguvu ya wanariadha wake mashuhuri.


