Hakuna mazungumzo ya mkataba mpya mpaka sasa kwa kapteni wa Yanga, beki Bakari Mwamnyeto ambaye mkataba wake umebakisha miezi Minne kumalizika.
Mwamnyeto alitua Yanga tangu Mwaka 2020 akitokea Coastal Union, kisha Mwaka 2024 akaongeza miaka miwili mkataba unaoisha Mwaka huu.
Ikumbukwe Simba SC ni timu iliyowahi kuvutiwa na Mwamnyeto, inawezekana Yanga wakichelewa kumbakisha, msimu ujao tukamshuhudia tena beki huyo akivaa uzi mwekundu.
