SMshambuliaji wa Uganda Cranes, Steven Desse Mukwala ameandika historia mpya baada ya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kutoka Uganda kwa sasa.
Mukwala analipwa dola 55,000 kwa mwezi (takribani shilingi milioni 220 za Uganda na zaidi ya milioni 140 za kitanzania)akiwa na klabu ya Al-Nassr Benghazi ya Libya ambayo amejiunga nayo akitokea Simba Sc ya Tanzania.
