Kiungo Malaika Meena amejiunga na klabu ya Ipswich Town FC Women inyoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza kwa mkopo akitokea klabu ya Bristol City inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza.
Malaika alijiunga na Bristol City Februari 2025 baada ya kumaliza masomo yake na kucheza soka la chuo nchini Marekani.
Alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu (2.5 years) wenye chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Timu / akademi alizopita Malaika Meena
1. Arsenal Academy – alianza kukuza kipaji chake hapo.
2. Chelsea Academy – akaendelea na maendeleo ya soka la vijana.
3. Wake Forest University (USA) – alicheza kwa takribani miaka mitatu na nusu kabla ya kurejea England.
4. Bristol City Women FC – amedumu kwa mwaka mmoja
Malaika Meena anahesabiwa kama mchezaji wa wa kimataifa wa Tanzania (Twiga Stars) ingawa hajawahi vaa jezi ya Tanzania na badala yake aliwahi kuiwakilisha England katika ngazi za vijana ikiwemo mwaka jana timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 23.
