Kisipika punguza maneno mengi subiri muda utaongea,mimi ni mwandishi ambe nafanya uchunguzi kabla ya kuzungumza….nakumbuka hata kwenye issue ya Chama ulisema vile kama unavyosema leo kwa Mpanzu..
Hans Raphael leo amejiwa juu na msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally "Semaji la CAF" kumjia juu Hans Raphael akishangaa maneno ya mchambuzi huyo wa Crown FM kudai kwamba mchezaji Elie Mpanzu licha kwamba anaichezea Simba lakini mapenzi yake yapo kwa Yanga.
Hata hivyo mchambuzi huyo kupitia ukurasa wa facebook, amemjibu akiandika maneno hayo katika utangulizi wa habari hizi.
