Meneja wa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally ametamba kama Ligi ya mabingwa Afrika ingeanza sasa basi Simba SC ingepata ushindi wa mechi sita mfululizo.
“Tulikuja hapa kwa ajili ya kupigania heshima ya Mnyama”
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally anasema kama hatua ya makundi ingeanza sasa, basi timu hiyo ingeshinda mechi zote sita.
Ahmed amezungumza hayo baada ya Simba kutoka sare na Petro Atletico kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
