Kocha wa timu ya Taifa ya Saudi Arabia, Herve Renard amedai kuwa anajutia uamuzi wake wa kuitosa timu ya Taifa ya Morocco mwaka 2019 licha ya kuwa na mkataba mrefu. Na kisha timu hiyo kufanya makubwa chini ya Kocha Walid Regragui ambaye alichukua nafasi yake.
"Sikupaswa kuondoka, nilikuwa na mkataba wa kuinoa Morocco hadi mwaka 2022, nikaondoka mwaka 2019 lakini hiyo ni sehemu ya makosa unayoweza kuyafanya kazini".
-Herve Renard, kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Saudi Arabia.
